Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari |
WATUHUMIWA wa utekaji wa basi la sumry katika tukio la wiki
iliyopita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Katavi wakiwamo wakimbizi
kutoka nchi jirani ya Burundi.
Jeshi la polisi mkoani Katavi limetoa taarifa kuwa jumla ya
watuhumiwa kumi na mbili wamekamatwa kwa tuhuma za kuliteka basi la kampuni ya
usafishaji ya Sumry High Class lenye namba T107BHT wiki iliyopita katika kijiji
cha Magamba wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kilometa nne toka Mpanda mjini.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Joseph Myovella
alisema Oktoba 26, 2012 kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakiuza simu za mkononi
zilizochukuliwa katika tukio la utekaji wa basi la Sumry ambapo baada ya
kuhojiwa walikiri na kuwataja waliokuwa nao.
Alisema katika upelelezi kwa kutumia tekionolojia ya
mawasiliano mtambo maalum uliweza kubaini kuwapo matumizi ya simu
zilizochukuliwa katika eneo la mkoa wa Katavi ndipo waliweza kufuatilia vipimo
na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiziuza simu hizo licha ya kuwa zilikuwa
zimebadilishwa laini zake.
“Kwakutumia tekinolojia tumeweza kuzisoma simu
zilizochukuliwa katika tukio hilo zikisomeka katika mtandao kuwa zinatumika
katika eneo la mkoa wetu wa Katavi tukaanza kuzifuatilia hadi tukafanikiwa
kuwakamata watuhumiwa moja baada ya wmingine hadi kufikia idadi ya kumi na
mbili” alisema Myovella.
Alifafanua kuwa hivi sasa bado jeshi lake linaendelea na
uchunguzi zaidi na hivyo majina ya watuhumiwa yatawekwa wazi mara baada ya
kukamilika upelelezi ambapo silaha zilizotumika zilikuwa ni mapanga, nondo na
fimbo.
Jeshi hilo lilitoa wito kwa wananchi kutokununua simu
zinazouzwa mitaani kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia kwenye mkubo wa
utekaji basi kwa sababu sasa hivi tekinolojia inayotumika inaonesha mtumiaji wa
simu iliyochukuliwa katika utekaji wa basin a mahali alipo mtumiaji kiasi
kwamba endapo mtu atanunua simu hiyo atakamatwa na kwa utaratibu wa upelelezi
atajumuishwa katika orodha ya watuhumiwa.
Alisema kati ya watuhumiwa hao kumi ni Watanzania na wawili
ni Raia wan chi jirani ya Burundi wanaoishi kama wakimbizi katika makazi ya
wakimbizi ya Katumba.
Blog hii itawaletea picha na majina ya watuhumiwa hao mara baada ya upelelezi wa polisi kukamilika
SHIRIKI KUWABAINISHA WATEKAJI WA BASI KWA KUTOA TAARIFA ZA SIRI KUPITIA NAMBA 0767 519989, 0784 519988 Jina lako na utambulisho wako ni siri kubwa kwetu.