Katibu Rukwa Press Club Sammy Kisika akisalimiana na kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda ofisini kwake jana. |
Kamanda wa jeshi la polisi akisalimiana na Mkufunzi wa habari wa mtandaoni Lukelo Mkami |
Willy sumia
JESHI la polisi mkoani Rukwa limeutaka muungano wa vyama vya
waandishi wa habari nchini UTPC kutoa mafunzo ya uandishi wa habari mtandani
kwa maaskari wake ili waweze kuwa na mchango bora kwa waandishi wa habari kwa
kutumia mitandao mkoani humo.
Akizungumza na mkufunzi wa tekinolojia ya habari za
mtandaoni Lukelo Mkami alipofika ofisini kwa kamanda wa polisi mkoa humo Jacob
Mwaluanda alisema kuwa mafunzo hayo yanarahisisha sana ufikishaji wa habari kwa
wananchi kwa muda mfupi zaidi badala ya kutegemea vyombo vya habari vya
kitaifa.
Mwaluanda alisema jana oktoba 18, 2012 kuwa katika mazingira
ya kiutendaji kazi katika mkoa wake jeshi lake linategemea sana uungwaji mkono
na ushuiriki mkubwa wa waandishi wa habari ili kufanikisha shughuli za jeshi la
polisi kuwatumikia wananchi kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo utaalamu
waliopewa waandishi wa habari mkoani humo ni muhimu sasa UTPC kuangalia
uwezekano wa kuwapa mafunzo kama hayo na vijana wake.
“Ukweli ni kuwa sisi jeshi la polisi tungependa pia mafunzo
kama haya yatufikie na sisi ili tujue nini kinachoendelea pamoja na
kuturahisishia kuwa na mawasiliano ya karibu na waandishi wa habari wetu wa
mkoani Rukwa.” Alisema Mwaluanda
Akizungumzia maboresho ya kiutendaji kazi ndani ya ofisi
yake kamanda wa polisi mkoani humo alisema ofisi yake inakusudia kubadili mfumo
wa utoaji habari kwa waandishi wa habari Press Release kwa kuanza kutuma moja
kwa moja katika mtandao kwa kutumia anwani za email ya mwandishi husika na
hivyo itasaidia kupatikana habari za polisi kwa wakati na haimulazimishi
mwandishi kuhudhuria kikao.
Mkufunzi wa mafunzo ya tekinolojia ya habari za mtandaoni,
Lukelo Mkami alisema kuwa licha ya kujifunza tekinolojia waandishi wa habari
pia wamefundishwa maadili ya uandishi wa habari zenye maadili katika mitandao
yao maarufu kama blogs ili kutofautisha blogs za wataalamu na za wasio na
utaalamu wa habari.
Alimsihi kamanda Mwaluanda kuwa na ukaribu na waandishi wa
habari siyo kwa ajili ya habari pekee bali pia katika suala zima la elimu kwa
umma juu ya suala la majukumu ya polisi kama vile polisi jamii, utii wa sheria
bila shuruti na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Katibu wa Rukwa Press Club, Sammy Kisika alisema umefika
sasa wa jeshi la polisi na waandishi wa habari mkoani Rukwa na Katavi kubadili
mwelekeo na kuanza ukurasa mpya wa kiutendaji kwa mshikamano zaidi ili kuongeza
kasi ya kuwahudumia wananchi wa mikoa hiyo na kusahau yaliyopita.
AJALI KWA UZEMBE AU BAHATI MBAYA |
UBEBAJI KAMA HUU NI HATARI |
BODA BODA MTATUMALIZA WATEJA WENU
WANANCHI mkoani Katavi wanalalamikia madereva wa pikipiki
maarufu kwa jina la bodaboda kwa kusababisha ajali za mara kwa mara kutokana na
kitendo cha kutokuwa na ujuzi wa kutumia chombo hicho na kuwakimbia polisi wa
usalama barabarani.
Kauli
hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa katika uzinduzi wa kamati mpya ya usalama
barabarani ya mkoa wa Katavi, kaimu kamanda wa polisi Mrakibu Mwandamizi wa
polisi Joseph Myovella alisema, ‘ukosefu wa elimu ya usalama barabarani ulichangia
baadhi ya majeruhi kupata ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza maisha’.
Watu
18 walikufa na wengine 215 kujeruhiwa katika jumla ya ajali 211 zilizotokea
katika kipindi cha miezi minne toka
kuanzishwa kwa mkoa Mpya wa Katavi kuanzia Julai mwaka huu. Myovela
alifafanua kwa kutaja takwimu.
Kati
ya ajali hizo waendesha pikipiki maarufu
kwa jina la boda boda wanatuhumiwa kusababisha jumla ya ajali 96 ambazo zinadaiwa kutokea kutokana na uzembe
wa kutojua sheria za usalama barabarani na kuwakimbia askari wanapotaka kuwapa
ushauri.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Lutengwe na Mwenyekiti wa kamati hiyo Nassoro Arfi
wakizungumza katika siku ya kuadhimisha siku ya usalama barabarani mwishoni mwa
wiki walilitaka jeshi la polisi
kujipanga vizuri ili kupunguza matukio
ya ajali za barabrani zinazotokea mara kwa mara mkoani humo na kunusuru
maisha ya watu.
Baadhi
ya madereva wa pikipiki mkoani humo ambao wamelipongeza jeshi la polisi kwa
jitihada za kuhakikisha ajali za barabrani zinapungua kwa kutoa mafunzo, walisema
kuwa kwa sasa wao watakuwa ni chachu ya kupunguza matukio ya ajali za
barabarani na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na hawatawakimbia tena
kwani kifo hakichagui.
No comments:
Post a Comment