Mnamo Oktoba 17,
2011 Mji wa Mpanda ulipokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliofika
kwa lengo la kushiriki katika Kongamano kubwa la Kimataifa la Uwekezaji ambalo
mwenyekiti wake alikuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete.
Hali ya maboresho ya kisekta baada ya kongamano la uwekezaji
lililofanyika Oktoba 17, 2011 katika Halmashauri ya Mji Mpanda katika kipindi
cha mwaka mmoja hadi Novemba 2012 ni kama ifuatavyo:-.
Katika Halmashauri ya mji Mpanda uwekezaji umekuwa ukiongezeka
katika kipindi cha mwaka 2011/12 kutokana na takwimu za maombi ya leseni na
maeneo ya uwekezaji kuongezeka kutoka waombaji wa leseni za biashara 40 katika
mwaka wa fedha 2010/11 hadi waombaji 211 wa leseni za biashara mbali mbali
katika kipindi cha Oktoba 2011 hadi Julai 2012.
Kuanzia julai 23, 2012
kitabu cha leseni kilichokuwepo kiliisha ambapo maelekezo ya wizara yalielekeza
kuwa halmashauri zisubiri utaratibu mpya wa leseni za biashara utakapotolewa.
Leseni zilizoombwa ni kwa ajili ya duka la dawa leseni mbili,
kuuza misumari leseni moja, spea za baiskeli leseni nne, kibanda cha simu
leseni moja, kuuza Oil leseni moja, Nyumba ya kulala wangeni leseni nne,
mgahawa leseni mbili, kuuza vocha leseni
nne, wakala wa M-pesa leseni tatu, duka la reja reja leseni 25 na vyombo vya
nyumbani leseni nane
Maombi mengine yalikuwa leseni ya stationary supplies, vyuma
chakavu, mitumba, nguo, viaa vya ofisini, ushuru wa mazao, kituo cha kurusha
matangazo ya radio ya fm, usafirishaji, vyombo vya pikipiki, vioo na vifaa
vyake, vifaa vya radio na runinga, vifaa vya ujenzi, vifaa vya magari, mashine
ya kusaga, kuuza gesi na mitambo yake ya kupikia, kununua na kuuza ng’ombe na
mashine ya kusaga
Pia ziliombwa
leseni za zahanati, udalali, uwakili, bima ya mali, bucha pamoja na kuuza simu
za mkononi
Aidha latila sekta ya mawasiliano kumekuwa na maboresho makubwa ya
mawasiliano kwa kutumia mitandao ambapo kuna zaidi ya blogs ishirini na mbili
katika mkoa wa Katavi hususani mjini Mpanda kati ya hizo tano zinamilikiwa na
kuendeshwa na waandishi wa habari waliopata mafunzo ya uendeshaji wa blogs,
mbili zinamilikiwa na Halmashauri na hivi sasa inatayarishwa website ya mkoa wa
Katavi baada ya kukamilika kwa website ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
ambayo makao yake makuu yako mjini Mpanda.
Aidha Halmashauri ya mji Mpanda wakati inajipanga kuwa Manispaa
imeanza mchakato wa kuwa na website yake mara baada ya kukamilika website ya
mkoa kutokana na kuwa na wataalamu wale wale wanaoanda website kwa ajili ya
taasisi za serikali ambao ni watumishi wa halmashauri mbili, ya Mji na
halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
Katika usafiri wa anga maboresho ya uwanja wa ndege yamechangia
kubadili sura ya mji wa Mpanda na kuongeza uchumi kwa wakazi wa mjini Mpanda
pamoja na kuwa na uhakika wa safari za ndege baada ya kuanza kwa usafiri wa
anga ambapo kampuni ya ndege ya Uric Air kuanza safari za Mpanda, Tabora,
Mwanza na Mbeya, Sumbawanga, Mpanda, Iringa na Dar Es Salaam.
Ifuatayo ni baadhi ya miradi iliyoibuliwa na wananchi, wawekezaji
na wadau wa maendeleo ya mkoa wa Katavi baada ya kongamano la uwekezaji katika
kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita katika eneo la Halmashauri ya Mji
Mpanda.
Miradi hiyo imegawanyika kisekta ambapo taarifa hii imechukua
miradi wakilishi ya mingine kwani sekta moja imekuwa na miradi zaidi ya mmoja
iliyoibuliwa na hivyo kuonesha sura ya mafanikio ya kongamano la uwekezaji
ambalo lilifanyika kwa mara ya kwanza mjini Mpanda enzi hizo ikiwa ni mkoa wa
Rukwa.
ASANTE VODACOMTZ |
DUBAI GUEST HOUSE MPANDA |
Nyumba hii ya kulala wageni
ya Dubai iko katika mtaa wa Majengo kata ya Kashaulili mjini Mpanda, ilianza
kujengwa 2011 ikiwa ni matunda ya msukumo wa uhitaji wa
nyumba za kulala wageni zenye hadhi ya kati na ya juu katika mji wa Mpanda mara
baada ya kongamano la uwekezaji.
Mradi huu umegharimu jumla ya
Shilingi 100,000,000/=
(milioni Mia moja) zikiwa ni fedha
zinazotokana na shughuli za kilimo na biashara zilizotolewa na mmiliki wa
nyumba hii ni ndugu IBRAHIM MAGOHA.
Nyumba hii ya
kulala wageni ina jumla ya vyumba 10 na inahudumia
wageni wa ndani na nje ya nchi tangu ikamilike mwezi Julai 2012
Tangu kuanza
kazi nyumba hii imekuwa ikijaza wageni vyumba vyote kila siku na kuwa na
uhakika wa kipato cha wastani wa shilingi 5,400,000/=
kwa mwezi.
Ni hoteli ya Kisasa iliyopo katika Mji wa
Mpanda kata ya Ilembo jirani na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda.
Hoteli hii ilianza kujengwa mwaka 2010 na kukamilika ujenzi wa
awali wa vyumba 29 vinavyojitegemea kila kimoja mnamo Aprili 2012 kutokana na
msukumo wa uhitaji wa malazi kwa wageni wa kimataifa katika mji wa Mpanda
Gharama za mradi huu ni zaidi ya shilingi milioni 800 ambapo ujenzi wa kumbi za
mikutano na mahitaji mengine ya malazi ya wageni unaendelea Mmiliki wa hoteli
hii ya kisasa ni Deusi Assenga na kampuni yake ya Assenga Association Co. Ltd ya Mpanda
Kipato cha
hoteli hii kwa wastani katika mwezi kwa vyumba vilivyokamilika kwa sasa ni
shilingi 6,500,000/=(milioni sita na
laki tano)
Ujenzi wa hoteli
hii ni chachu ya kuinua kipato cha Mji wa Mpanda pamoja na kuuwezesha mji wa
Mpanda kupokea wageni wa aina zote bila kikwazo cha malazi ya uhakika.
Kufunguliwa kwa tawi la benki ya CRDB
kumetokana na hali halisi ya uhitaji wa huduma za kibenki katika mkoa wa Katavi
kutokana na kukua na biashara na mzunguko wa fedha katika jamii ya wakazi wa
mkoa wa Katavi.
Tawi la CRDB Mpanda lililofunguliwa miezi miwili kabla ya
kongamano la uwekezaji ni moja ya matunda ya kongamano kwani uwepo wa kongamano
ni sehemu ya msukumo wa kufunguliwa mapema benki hii ili washiriki na wadau wa
maendeleo waweze kupata huduma ya kibenki kutoka CRDB.
Licha ya kuwa na uchanga katika kazi ya kibenki, benki ya CRDB tawi la Mpanda imepeta ongezeko
la wateja katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka wateja 1,000 mwezi
Septemba 2011 hadi wateja 5,700 Novemba
6, 2012 ikiwa ni ishara ya kuwepo kwa
hitaji la upanuzi wa benki hii hivi karibuni kutokana na ongezeko la wateja.
Changamoto inayoikabili benki ya CRDB Mpanda ni kutopatikana kwa hati za
umiliki wa nyumba au ardhi kwa wateja wake ili waweze kukopesheka na kuinua
kipato cha wateja wake.
Mwananchi duka la dawa lipo katika mtaa wa
kanisa la Moravian mjini Mpanda katika jengo la kitegauchumi la kanisa hilo,
duka hili linatizamana na ofisi za kampuni ya mabasi ya Sumry katika soko la Buzogwe
Duka hili lilianza Juni 2012 baada ya kukamilika kwa ukarabati wa
jingo ambapo mmiliki wa duka hili anaitwa Dr Lugata mkazi wa mjini Mpanda
Maendeleo ya mauzo yamekuwa yakipanda kadiri siku zinavyosonga
mbele kutokana na ugeni wa eneo husika wananchi wengi bado hawajajua kama kuna
duka la dawa za binadamu changamoto ambayo mmiliki wa duka hili anasema
inapungua siku hadi siku.
Baada ya kongamano mmiliki wa duka la Mwananchi ndipo alipopata
wazo la kuweka duka hilo kutokana na msongamano wa watu mjini Mpanda na kuwepo
kwa mahitaji makubwa ya huduma ya dawa baridi.
Katika kile kinachoonekana kuwa ni matunda ya wazi ya kongamano la uwekezaji lililofanyika Oktoba 17, 2011 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda bila shaka yoyote ni kuibuka kwa usafiri wa mabasi kutoka Tabora mjini hadi Mpanda mjini.
Kwa kipindi cha miongo kadhaa kumekuwa hakuna usafiri wa bara bara
kutoka mjini Tabora kuelekea mjini Mpanda kwa kutumia mabasi ya kisasa na
badala yake wananchi waliokuwa wakisafiri katika ya mikoa ya Rukwa enzi hizo na
Tabora walilazimika kuzunguka Mbeya au kutumia usafiri wa garimoshi.
Mara baada ya kongamano kupita mji wa Mpanda ulianza kupokea
mabasi kila siku na kuongeza idadi ya mabasi yanahudumiwa na stendi kuu ya
mabasi mjini Mpanda na kuonekana kuelewa kwa stendi hiyo iliyobuniwa kwa ajili
ya kuhudumia mabasi ya mikoani.
Kila siku kuna mabasi yanayoondoka kuelekea mjini Tabora toka
Mpanda na pia kunamabasi yanakuja Mpanda kutoka mjini Tabora na wakati mwingine
mawili kwa siku moja na safari moja.
Katika
kuboresha kilimo kwanza Halmashauri ya mji iliwaongoza wananchi wa Kakese
kuibua Mradi wa ujenzi wa ghala ambao uliibuliwa na wananchi wa kijiji cha
Mbugani Januari 2012 kupitia zoezi la fursa na vikwazo vya maendeleo (O &
OD) na kuanza ujenzi mwezi Mei 2012.
Mradi
huu umegharimu jumla ya shilingi za kitanzania 62,890,000/= kwa ufadhili wa
mpango wa maendeleo ya kilimo wilaya (DADPS) na baada ya kukamilika mwezi
Desemba 2012 ghala hili litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 250 za mpunga
Wakizungumza
kijijini hapo juu ya matumaini yao katika ghala ya mazao wananchi hao walisema
kuwa walikuwa wanalazimika kuuza mazao kwa ya chini kutokana na ukosefu wa
ghala la kutunzia mazao pamoja na kuwa wanategemea kutumia mtindo wa kuuza
mazao ya katika ghala hilo kwa kutumia utaratibu wa stakabadhi ghalani
Uwepo wa barabara mbili za lami kati kati ya mji ni sehemu ya
kivutio cha mji wowote utofauti wa mji wa mpanda ni kuwa na mandhari nzuri ya
njia mbili iliyobebwa na maua yaliyopanda kwa ustadi mkubwa pamoja na mapambo ya matangazo ya kampuni ya
simu ya Vodacom
Vodacom Tanzania iliamua
kufanya mazungumzo na Halmashauri ya mji Mpanda kuwa na maboresho ya njia mbili
eneo la kati kati ya Mji maarufu kama Buzogwe ili kuwa na sura ya mji yenye
mfano wa pekee baada ya kongamano la uwekezaji la oktoba 17, 2011
Ni dhahiri kuwa bila kongamano hilo Vodacom wasingeiona barabara
mbili kama inahitaji kuwekewa mabango yake na sasa imekuwa kama maua yaliyoko
katika makao makuu ya mkoa wa Katavi.
SEMIU PHAMACY ya mjini Mpanda imeteuliwa na Bima ya Taifa
ya Afya kuwa wakala wake katika mkoa wa katavi baada ya kubaini mahitaji ya
mkoa huo kuwa makubwa kutokana na wingi wa mahitaji ya huduma hiyo kuwa kubwa.
Mmiliki wa Semiu Phamacy, Adrian Siwalima alisema kuwa alianza
duka la dawa oktoba 2010 lakini baada ya kupita kongamano la uwekezaji alipata
wageni kutoka shirika la Bima ya afya nchi wakitaka kufanya mazungumzo naye
aweze kuwa wakala wa shirika hilo katika mkoa wa Katavi.
Alisema alikubaliana nao kufanya maboresho ya jingo lake ili
liweze kumudu mahitaji ya huduma husika ambapo amefanya marekebisho ya jingo na
kuwa na hadhi ya Bima ya Afya kwa kufuata ramani ya shirika kwa gharama ya
shilingi milioni ishirini (20,000,000)
Alisema baada ya kuanza mauzo ya dawa baridi katika duka hilo la
Bima mapato yamefikia shilingi milioni kumi (10,000,000) kwa mwezi kutokana na ugeni wa huduma hiyo ambapo
alibainisha kuwa kwa ongezeko la watu lilivyo katikam mkoa wa katavi mauzo
yatapanda mara nne au zaidi ya hapo.
Baada ya kongamano la uwekezaji la mwaka jana,
miezi michache kumeibuka ujenzi wa mitambo ya kurushia matangazo ya radio
miwili kwa masafa ya fm katika mji wa Mpanda yaliko makao makuu ya mkoa wa
Katavi
Ipo Mpanda Radio Fm inayomilikiwa na mfanyabiashara wa mjini
Mpanda Aleem Kanji iliyopo katika eneo la Mpandahoteli jirani na kiwanda cha
Madini cha TPM inayotarajia kuanza wakati wowote baada ya kupata kibali kutoka
tume ya mawasiliano kwani ujenzi ulishakamilika bado kibali cha kuanza kazi
baada ya kukaguliwa na wahandisi wa mitambo ya radio na elektroniki kutoka
TCRA.
Aidha kipo kituo cha Radio cha Pamoja radio Fm kinachomilikiwa na
Mkazi wa Mpanda mjini John Malac ambacho kimekamilika ujenzi kinachosubiriwa ni
kibali kutoka tume ya mawasiliano nchini TCRA baada ya marekebisho
yalioainishwa na wahandisi kutoka tume. Kituo hiki kipo eneo la Kawajense
jirani na ofisi ya Chama cha msingi cha tumbaku LATCU ambapo mwekezaji ameamua
kuanza na jingo lililokuwa likitumika kama nyumba ya kuishi na kubadili
matumizi yake.
Baada ya kongamano ndugu Omonyo
mkazi wa kijiji cha Kakese Mbugani
aliamua kuwekeza katika sekta ya maji katika kijiji cha Kakese Mbugani
kwa lengo la kujipatia kipato kutoka kwa wananchi
Mradi huu umeweza kuondoa kero ya
ukosefu wa huduma ya maji safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu katika kijiji
cha Kakese Mbugani ambapo kilio cha shida ya maji kilikuwa kikubwa kutoka kwa
wakazi wa kijiji hicho.
Kwa
maelezo yake ni kuwa aliamua kuwa na mradi wa kuuza maji katika visima viwili virefu vya maji ili kuboresha
huduma ya upatikanaji wa maji hapa kijijini pamoja na kujiongezea kipato na ili
kutimiza lengo aliamua kuwatumia wataalamu wa maji kutoka halmashauri ya mji.
Mradi
huu umegharamiwa na mmiliki mwenyewe ambapo mpaka sasa mradi huu umetumia shilingi 8,648,500/= hadi kukamilika kwa
asilimia mia moja na makusanyo kwa mwezi ni wastani wa shilingi 120,000/=
KIWANDA CHA
KUYEYUSHIA MADINI TPM - MPANDA
Ujenzi
wa kiwanda cha kuyeyushia madini mjini Mpanda umeongeza ajira na kipato kwa
baadhi ya vijana mjini Mpanda na nje ya Mpanda kutokana na ongezeko la ajira
katika kiwanda cha TPM (Tanzania Pema Mining).
Pia
mandhari ya mji wa Mpanda imeongezeka ubora na kuwa na uhakika wa soko la
madini kwa wachimbaji wadogo awali
walikuwa wakiuza dhahabu kwa bei ndogo kutokana na kukosekana kwa soko la
uhakika mjini Mpanda na katika
Katika
eneo lilojengewa kiwanda kuna biashara ya mama lishe ambao wamekuwa wakipata
kipato kwa njia ya kuuza chakula kwa wafanyakazi wa kampuni ya TPM ambao
wanatoka mbali na eneo kiwanda kilipo
Pamoja
na kuwa TPM ilianza kabla ya kongamano la uwekezaji ilikuwepo lakini
halmashauri inaamini kuwa uwepo wa kiwanda cha TPM katika mji wa Mpanda ni
kivutio kikubwa kwa wawekezaji wengine wa ndani na nje kutokana na kuwepo kwa
dhana ya kutokuwezekana mambo katika sehemu kama za kwetu kwa imani tu
Kuasisiwa kwa mkoa Mpya kumekuja na kuasisiwa
kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Kilimo ambacho kimepewa jina linalobeba jina la
Mkoa na Hifadhi ya Taifa iliyoko katika mkoa yaani Katavi.
Chuo kikuu cha kilimo ni sehemu
ya juhudi ya kuwekeza katika Elimu ambapo Halmashauri inaamini kuwepo kwa chuo
kikuu kinachomilikiwa na kuendeshwa na Halmashauri kutaiwezesha jamii ya wana
Katavi kuwa na maendeleo endelevu na yenye tija katika kuboresha maisha ya
wananchi
Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Katavi
kitaweza kuchangia katika suala zima la elimu ya juu kwa vijana wanaokosa
nafasi katika vyuo vikuu vingine kutokana na kuwa ukanda wa Ziwa Tanganyika ni
ukanda pekee usio kuwa na chuo kikuu kinachotoa taaluma mbali mbali kwa vijana
na wahitimu wa kidato cha sita.
Wakazi wa mji wa
mpanda mkoa mpya wa katavi wameanza kupata huduma ya usafiri wa
ndege tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba 2012.
Usafiri huo umeanza
kupatikana kufuatia kampuni ya ndege ya URIC AIR kuanza safari ya kusafirisha
abiria kutoka Mjini Mpanda kuelekea mikoa mingine.
Ndege hiyo ya kampuni
ya URIC AIR itakuwa ikifanya safari zake kila siku katika mikoa ya Mwanza,
Katavi na Kigoma ambapo awali wakazi wa mkoa wa Katavi walikuwa wakilazimika
kufuata usafiri wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa umbali wa kilometa 240
au mkoani Tabora kilometa 366.
Uwanja wa ndege wa
mpanda ambao ni miongoni mwa viwanja vya ndege vilivyotengenezwa kwa kiwango cha
lami toka ulipokamilika ulikuwa ukitumiwa na makampuni mbali mbali kutua kwa
ndege
Uanzishwaji wa safari
za ndege katika mkoa wa Katavi utarahisisha watalii na wawekezaji kufika kwa
urahisi mkoani Katavi kwani hapo awali usafiri ulio kuwepo ni wa magari na
garimoshi.
KILIMO KWANZA YAJA NA MAPYA MPANDA MJINI
Mradi huu wa matrekta uliibuliwa
na vikundi viwili vya wakulima katika
kata za Ilembo na Mpanda Hoteli katika msimu wa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa
lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao
kwa wakulima ambapo matrekta haya yamekuwa yakiongeza ufanisi katika kilimo
pamoja na usafirishaji kwa wananchi wenye pato la chini.
Mradi huu unagharana ya
shilingi 75,523,160.kati ya hizo
Halmashauri ya mji Mpanda imechangia shilingi 1,372,217.00 na vikundi
vimechangia jumla ya shilingi 8,200,000.00, mfuko wa maendeleo ya kilimo ASDP
umechangia kiasi kilichosalia kwa kwa ajili ya vikundi viwili vya Muungano
Farmers Association na Mshikamano Agricultural Group
Katika kuboresha mazingira ya
kuhudumia wananchi Halmashauri ya Mji wa Mpanda imefanikisha ujenzi wa ofisi ya
Mtendaji wa kata Kawajense na kuondoa kero ya ukosefu wa ofisi kwa watendaji na
Diwani wa kata hiyo.
Mradi huu wa ujenzi wa ofisi ya
Kata ya Kawajense uliibuliwa na wananchi katika msimu wa mwaka wa fedha
2011/2012 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuongeza ufanisi
katika kuwahudumia wananchi kwa gharama ya shilingi 31,001,428 ambapo Serikali
kuu imetoa shilingi 21,221,969.50 na wananchi wamechangia jumla ya shilingi
6,019,000
Kata ya Kawajense
imekuwa na mahitaji makubwa ya ofisi kutokana na kuwa na eneo la viwanja vipya
vya kujenga nyumba vingi kuliko kata nyingine na hivyo kata hii inapokea wageni
wengi kila siku hali inayoashiria mahitaji ya ofisi kwa ajili ya kutoa huduma
kwa ufanisi.
Halmashauri ya
Mji Mpanda inajianda kuendelea na ujenzi wa karakana ya kikundi cha walemavu
cha kutengeneza viatu iliyopo katika kata ya Ilembo .
Mradi wa ujenzi
wa jengo hili la karakana ulianza mwezi Februari mwaka 2009 kwa lengo la kutoa
mafunzo kwa watu wenye ulemavu ili watakapohitimu mafunzo hayo waweze kujiajiri
wao wenyewe lakini baada ya kongamano la uwekezaji kikundi cha walemavu waasisi
wa karakana hiyo kupitia TASAF waliona umuhimu wa kuanza mikakati ya
kukamilisha karakana hiyo ili waweze kuanza uzalishaji kutokana na uwepo wa
soko kubwa.
Kupitia halmashauri
kikundi hicho kimepata msaada wa kumaliziwa na halmshauri ya mji ili kufikia
lengo kabla soko la viatu vya kutengenezwa hapa mjini halijaingiliwa na
wazalishaji wengine ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Joseph Mchina
alisema kuwa atahakikisha karakana inakamilika kipindi kifupi kijacho kabla ya
Oktoba 2013 kwa kutumia fedha za makusanyo ya ndani.
Mradi huu
unagharamiwa na wafadhili mbalimbali ambapo mfuko wa maendeleo ya jamii nchini
TASAF Umechangia kiasi cha shilingi 9,090,909.90
na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
amechangia shilingi 500,000/=, Mpaka mradi kukamilika
utagharimu kiasi cha shilingi 24,000,000/=
na halmashauri itachangia gharama zilizobakia ili karakana ikamilika
Katika kuboresha miundombinu ya mji wa Mpanda
Halmashauri ya mji iliamua kuweka mazingira mazuri ya miundombinu katika maeneo
mbalimbali za mji wa Mpanda ikiwa ni pamoja na barabara ya duara (Ring Road)
katika njia ya kwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi kwa kiwango cha lami.
Mradi huu wa ujenzi wa
barabara mbili kwa kiwango cha changarawe ulianza mwezi Aprili 25,2012 na
unatarajia kukamilika Septemba 25, 2012 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya
barabara za mjini Mpanda makao makuu ya mkoa wa Katavi.
Mradi huu unagharamiwa
na Serikali kuu kwa Tsh. 100,000,000/= ambapo mpaka kukamilika kwa kiwango cha
lami zitatumika kiasi cha shilingi 98,463,800/=
Katika kuahakikisha uwekezaji katika sekta ya kilimo
unakuwa wa manufaa na wa uhakika baadhi ya makampuni yanayowekeza katika kilimo
cha tumbaku mkoani Katavi yameanza kujenga maghala ya kuhifadhia mazao yao ili
yaweze kuwasaidia katika kuhifadhi mazao.
Kampuni
ya kununua tumbaku ya Dmoni ya Morogoro imeamua kuanza kuwekeza katika zao la
tumbaku katika mkoa wa Katavi kwa kununua tumbaku kutoka vyama vya msingi kama
yalivyofanya makampuni ya TLTC, ATTT na PREMIUM.
Mradi
huu una gharama ya shilingi milioni mia tano hadi kukamilika kwa ujenzi wake na
ghala hili linatarajia kuanza kutumika
mwakani ambapo lina uwezo wa kuhifadhi tani laki tatu na nusu kwa za mazao kwa
wakati mmoja.
Kuanzishwa
kwa Chuo kikuu huria tawi la Mkoa wa Katavi kumetoa fursa ya pekee kwa wananchi
wa mkoa huu kuweza kujipatia elimu ya Chuo kikuu kwa gharama nafuu tena katika
mazingira yao wenyewe.
Uwekezaji
huu wa ni muhimu sana katika kusukuma maendeleo ya wana Katavi kwani Elimu
inayotolewa itawasaidia wasio na uwezo wa kifedha na nafasi kupata elimu ya
chuo kikuu kwa gharama ndogo na katika mazingira yanayomuwezesha mwananchi wa
kawaida kumudu gharama na mahitaji.
Halmashauri
ya Mji imekuwa ikiwahamasisha wananchi na wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za
serikali na zisizo za Kiserikali na kukitumia Chuo Kikuu Huria kujipatia elimu
ya Chuo kikuu kwa kutumia mikutano na vikao mbali mbali vya Halmashauri.
Maboresho makubwa ya uwanja wa ndege wa Mpanda
maarufu kama uwanja wa Kashaulili umefikia hatua ya kiwango cha lami kwa upande
wa njia ya ndege na maegesho yake
Kutokana na kuboreshwa kwa uwanja huo sasa ndege
zenye uwezo wa kubeba abiria 72 zinaweza kutua katika uwanja huo kwa kipindi
chote cha mwaka bila kujali masika au kiangazi
Kukamilika kwa uwanja huu kumeanza kutoa matunda
makubwa kwa kuvutia wawekezaji wakubwa na wa kati kuja kuanza shughuli za
uwekezaji katika mkoa wa Katavi pamoja na kuibua shughuli mpya za kiuchumi
ambazo hapo awali hazikufikirika kama zinawezekana katika mji wa Mpanda na mkoa
kwa ujumla.
Baadhi ya shughuli hizo zimewagusa wananchi wa
kawaida na nyingine zinawanufaisha pia wawekezaji wengine wa ndani na nje ya
mkoa wetu wa Katavi kama vile uanzishwaji wa safari za ndege kwa safari za
Kigoma Mpanda Kigoma, Mwanza Kigoma Mpanda na Mpanda Kigoma Mwanza ni sehemu ya
faida za kuwepo uwanja bora wa ndege.
HALMASHAURI YA MJI MPANDA YATENGA EKARI 600 ZA
KIUCHUMI
Ili kuhakikisha kuwa shughuli za kiuchumi zinapata
nafasi katika kipindi cha mapinduzi ya kiuchumi katika mkoa wa Katavi,
halmashauri ya mji Mpanda imeandaa ekari mia sita(600) kwa ajili ya eneo maalum
la kiuchumi ( Special Economic Zone) katika eneo linalopakana na mtaa wa
Airtel.
Eneo hilo litakuwa maalumu kwa ajili ya wawekezaji
wa huduma za uwanja wa ndege kama vile maduka vinyago, maduka makubwa
(Supermarket), mahoteli na nyumba za kulala wageni zenye hadhi ya kimataifa.
Katika eneo hili kutakuwa na ofisi za makampuni
yanayofanya kazi ya kusafirisha watalii katika maeneo yetu ya Kitalii na
hifadhi ya taifa ya wanyama ya Katavi.
No comments:
Post a Comment