Saturday, November 10, 2012

Breaking News

MASIKINI AFANDE CHACHA

AJIMALIZA KWA RISASI KISA TOFALI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri A. Kidavashari
ASKARI mmoja wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi amefariki dunia papo hapo baada ya kujipiga risasi mchana leo Novemba 10, 2012 katika eneo la Nsemulwa kwa Mkumbo mjini Mpanda.

tukio hilo limetokea katika eneo linalotumika kufyatulia tofali ya kujengea ambapo imeelezwa kuwa askari aliyejiua ametajwa kwa jina moja la Chacha wa kikosi cha kutuliza ghasia mjini Mpanda baada ya kukuta mama mmoja akisombelea tofali alizokuwa amenunua kutoka kwa muuzaji wa tofali.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Joseph Myovella amesema askari huyo alikuwa katika shughuli binafsi majira ya mchana alikwenda kuangalia tofali alizonunua katika mtaa wa Nsemulwa kwa Mkumbo na alipofika katika eneo alilonunulia tofali alimkuta mama mmoja akisombelea tofali hizo kwa madai kuwa ni za kwake na yeye ameuziwa tofali hizo ndipo askari huyo alirejea kituo cha polisi Mpanda mjini na kuchukua silaha aina ya SMG na kuondoka kuelekea alikokuwa amenunulia tofali.

imeelezwa kuwa alipofika eneo la tofali alimkuta mama huyo akiendelea na kazi ya kusomba tofali ndipo alimpiga risasi tatu tumboni, kifuani na ubavuni na kisha akapiga simu kituo cha polisi na kueleza kuwa ameua mtu na yeye anajiua

baada ya kupiga simu askari huyo alijipiga risasi sehemu za koromeo, kidevuni na sehemu za kifuani na kufariki papo hapo

hali ya majeruhi imeelezewa kuwa bado ni mbaya anaendelea kupata huduma katika hospitali ya wilaya ya Mpanda.

1 comment:

  1. Get admission into any university or college all over the world http://www.xbizy.com

    ReplyDelete