Friday, October 26, 2012

WATEKAJI WA BASI LA SUMRY KATAVI MBARONI


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari

WATUHUMIWA wa utekaji wa basi la sumry katika tukio la wiki iliyopita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Katavi wakiwamo wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi.
Jeshi la polisi mkoani Katavi limetoa taarifa kuwa jumla ya watuhumiwa kumi na mbili wamekamatwa kwa tuhuma za kuliteka basi la kampuni ya usafishaji ya Sumry High Class lenye namba T107BHT wiki iliyopita katika kijiji cha Magamba wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kilometa nne toka Mpanda mjini.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Joseph Myovella alisema Oktoba 26, 2012 kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakiuza simu za mkononi zilizochukuliwa katika tukio la utekaji wa basi la Sumry ambapo baada ya kuhojiwa walikiri na kuwataja waliokuwa nao.
Alisema katika upelelezi kwa kutumia tekionolojia ya mawasiliano mtambo maalum uliweza kubaini kuwapo matumizi ya simu zilizochukuliwa katika eneo la mkoa wa Katavi ndipo waliweza kufuatilia vipimo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiziuza simu hizo licha ya kuwa zilikuwa zimebadilishwa laini zake.
“Kwakutumia tekinolojia tumeweza kuzisoma simu zilizochukuliwa katika tukio hilo zikisomeka katika mtandao kuwa zinatumika katika eneo la mkoa wetu wa Katavi tukaanza kuzifuatilia hadi tukafanikiwa kuwakamata watuhumiwa moja baada ya wmingine hadi kufikia idadi ya kumi na mbili” alisema Myovella.
Alifafanua kuwa hivi sasa bado jeshi lake linaendelea na uchunguzi zaidi na hivyo majina ya watuhumiwa yatawekwa wazi mara baada ya kukamilika upelelezi ambapo silaha zilizotumika zilikuwa ni mapanga, nondo na fimbo.
Jeshi hilo lilitoa wito kwa wananchi kutokununua simu zinazouzwa mitaani kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia kwenye mkubo wa utekaji basi kwa sababu sasa hivi tekinolojia inayotumika inaonesha mtumiaji wa simu iliyochukuliwa katika utekaji wa basin a mahali alipo mtumiaji kiasi kwamba endapo mtu atanunua simu hiyo atakamatwa na kwa utaratibu wa upelelezi atajumuishwa katika orodha ya watuhumiwa.
Alisema kati ya watuhumiwa hao kumi ni Watanzania na wawili ni Raia wan chi jirani ya Burundi wanaoishi kama wakimbizi katika makazi ya wakimbizi ya Katumba.
Blog hii itawaletea picha na majina ya watuhumiwa hao mara baada ya upelelezi wa polisi kukamilika
SHIRIKI KUWABAINISHA WATEKAJI WA BASI KWA KUTOA TAARIFA ZA SIRI KUPITIA NAMBA 0767 519989,  0784 519988 Jina lako na utambulisho wako ni siri kubwa kwetu.

Wednesday, October 24, 2012

CHIMBUKO LA UKRISTO AFRIKA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA






























Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga Mhasham Askofu Charles Karolo Msakila enzi za uhai wake






Hapa ndio chimbuko la Ukatolikia na Ukristo Afrika ya Kati, Mashariki na Kusini mwa Afrika, Karema








Fort Leopard Karema port along Lake Tanganyika














Wasiliana nasi kwa email willysumia@gmail.com pia soma katika www.sumiampanda.blogspot.com
 WAWEZA KUPIGA SIMU YA KIGANJANI 0767 519989 //0784519988//0715519988