Thursday, October 18, 2012

BLOGGERS VS RPC RUKWA

Mkufunzi wa uandishi wa habari mtandaoni Lukelo Felix Mkami akisalimiana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa jana mara baada ya kuwasili ofisini kwake mjini Sumbawanga.


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaluanda

Katibu wa Rukwa Press Club, Sammy Kisika akiagana na Kamanda wa polisi mkoani Rukwa ofisini kwake jana.



Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa akiwasindikiza waandishi wa habari nje ya ofisi yake baada ya kuzungumza nao jana juu ya uandishi wa habari za Mtandao Blogs.

JESHI la polisi mkoani Rukwa limeutaka muungano wa vyama vya waandishi wa habari nchini UTPC kutoa mafunzo ya uandishi wa habari mtandani kwa maaskari wake ili waweze kuwa na mchango bora kwa waandishi wa habari kwa kutumia mitandao mkoani humo.
Akizungumza na mkufunzi wa tekinolojia ya habari za mtandaoni Lukelo Mkami alipofika ofisini kwa kamanda wa polisi mkoa humo Jacob Mwaluanda alisema kuwa mafunzo hayo yanarahisisha sana ufikishaji wa habari kwa wananchi kwa muda mfupi zaidi badala ya kutegemea vyombo vya habari vya kitaifa.
Mwaluanda alisema jana oktoba 18, 2012 kuwa katika mazingira ya kiutendaji kazi katika mkoa wake jeshi lake linategemea sana uungwaji mkono na ushuiriki mkubwa wa waandishi wa habari ili kufanikisha shughuli za jeshi la polisi kuwatumikia wananchi kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo utaalamu waliopewa waandishi wa habari mkoani humo ni muhimu sasa UTPC kuangalia uwezekano wa kuwapa mafunzo kama hayo na vijana wake.
“Ukweli ni kuwa sisi jeshi la polisi tungependa pia mafunzo kama haya yatufikie na sisi ili tujue nini kinachoendelea pamoja na kuturahisishia kuwa na mawasiliano ya karibu na waandishi wa habari wetu wa mkoani Rukwa.” Alisema Mwaluanda
Akizungumzia maboresho ya kiutendaji kazi ndani ya ofisi yake kamanda wa polisi mkoani humo alisema ofisi yake inakusudia kubadili mfumo wa utoaji habari kwa waandishi wa habari Press Release kwa kuanza kutuma moja kwa moja katika mtandao kwa kutumia anwani za email ya mwandishi husika na hivyo itasaidia kupatikana habari za polisi kwa wakati na haimulazimishi mwandishi kuhudhuria kikao.
Mkufunzi wa mafunzo ya tekinolojia ya habari za mtandaoni, Lukelo Mkami alisema kuwa licha ya kujifunza tekinolojia waandishi wa habari pia wamefundishwa maadili ya uandishi wa habari zenye maadili katika mitandao yao maarufu kama blogs ili kutofautisha blogs za wataalamu na za wasio na utaalamu wa habari.
Alimsihi kamanda Mwaluanda kuwa na ukaribu na waandishi wa habari siyo kwa ajili ya habari pekee bali pia katika suala zima la elimu kwa umma juu ya suala la majukumu ya polisi kama vile polisi jamii, utii wa sheria bila shuruti na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Katibu wa Rukwa Press Club, Sammy Kisika alisema umefika sasa wa jeshi la polisi na waandishi wa habari mkoani Rukwa na Katavi kubadili mwelekeo na kuanza ukurasa mpya wa kiutendaji kwa mshikamano zaidi ili kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi wa mikoa hiyo na kusahau yaliyopita.

No comments:

Post a Comment